Saikolojia inavyotibu tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni!






Saikolojia inavyotibu tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni!


Miongoni mwa matatizo makubwa kabisa yanayowakabili wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kuwa, wanaume saba kati ya kumi wanakasoro hii.
Malalamiko yanayotolewa na baadhi yao yanaonesha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba.
Hata hivyo, kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la pili na kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya wanawake limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi.
Ni ukweli usiopingika kuwa, mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani humwacha njia panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana.
Hali hii inatokana na maumbile ya uume wa mwanaume ambao husinyaa mara baada ya kuhitimisha mbio zake, lakini kwa mwanamke kuwahi si tatizo, kwani hakumfanyi ashindwe kumsindikiza mwenzake hadi kileleni.
Utofauti huu ndiyo unaowafanya wanaume wahuzunike zaidi wanapokabiliwa na janga hilo kiasi cha kufikia hatua ya kwenda kwa waganga/matabibu ili iwasaidie kuepuka balaa ya kutoka uwanjani na aibu.
Ingawa kumekuwa na mafanikio katika tiba za kisayansi, lakini bado wanaume wameshindwa kupata ukombozi wa kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta wakijiongezea mzigo wa fikra kwa kuzitumaini zaidi dawa au kuzitumia na kupata matokeo mabaya zaidi ya kuishiwa nguvu kabisa.
Kwa kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na madhara yachipukiayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo kwa kutumia kanuni za kisaikolojia na mafanikio yasiyo na madhara yakapatikana.
Wataalamu wa kisaikolojia wanatambua kuwa kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini. Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili, bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mapenzi kilichopokelewa kwenye ubongo unaojihusisha na hisia.
Ushauri wa masuala ya kimaisha na matatizo yote yanayohuzunisha unatolewa, Inaelezwa kuwa, akili ikishiba vigezo na kutuma taarifa zenye usahihi kwenye mwili viungo hupokea hisia na kuanza kusumbua. Kwa msingi huo kama tunataka kufika kileleni mapema au kuchelewa lazima tucheze zaidi na akili kuliko mwili.
Katika hali ya kawaida nguvu ya kupenda inayomwingia mtu huwa kubwa, lakini suala la kupunguza ukubwa wa hisia lazima lipewe kipaumbele. Jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wenye
tatizo la kufika kileleni mapema ni kuwa na PUPA ya kufanya mapenzi.
Wengi wao hupokea hisia zilizokuzwa na kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo la ndoa. Saikolojia inaelekeza kuwa ili mwanaume achelewe kumaliza, lazima apunguze mhemko unaotokana na kuona, kuhisi na kupagawishwa na staili au chombezo toka kwa mwanamke.
Anachotakiwa kufanya ni kutumia zaidi ya dakika 20 kufanya maadalizi na mpenzi wake kabla ya kuanza tendo. Hii itasaidia kuufanya mhemko wake ushuke na kumuongezea muda wa kumaliza.
Aidha mbinu ya kuidanganya akili lazima itumike ili kuzima taarifa za juu za uzuri wa mwanamke, maumbile na raha ya starehe isipokelewe kwa nguvu kubwa mwilini.
Hii ikiwa na maana kuwa kuna kipindi inabidi fikra za mwanume zisihamasike sana kwenye tendo badala
yake iletwe mawazoni hali ya kawaida, si ile ya kuweweseka na kuhema hema hovyo.

YAFUATAYO NI MAELEKEZO YA MSINGI YA KUFANYA, ILI MTU ASIFIKE KILELENI MAPEMA:

Mume na mke wanapoingia katika uwanja wa mapenzi wakae kwanza kwa muda, huku wakiwa wamejiachia na mavazi mepesi.
Pili wacheze michezo mingi kwa muda mrefu bila kuanza kazi yao. Wakiwa kwenye hamasa hizo wasiwe kimya bali wazungumze na kuulizana maswali ya kimahaba.

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kuthibitisha kama mtu anakupenda kwa dhati

Athari za kujichua kwa wanaume na wanamke waliopo kwenye mahusiano

Mazoezi ya kuufanya uume usimame kwa muda mrefu na uchelewe kufika kileleni mapema