Mazoezi ya kuufanya uume usimame kwa muda mrefu na uchelewe kufika kileleni mapema
Mazoezi ya kuufanya uume usimame kwa muda mrefu na uchelewe kufika kileleni mapema
Misuli inayohusika na nguvu za kiume na kuwahi kumaliza wakati wa tendo la kufanya mapenzi huitwa “puboccugeous Muscle” maarufu inajulikana kama Pelvic Muscle.
Misuli hii inapokuwa dhaifu, uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu na kuchelewa kukojoa wakati wa kufanya mapenzi huwa mdogo.
Zoezi lenye uwezo wa kuongeza nguvu ya misuli ya uume, linaloweza kuufanya uume kusimama kwa muda mrefu, bila kusinyaa wala kuchoka, hili ni zoezi kama mfano wa zoezi lolote la kunyanyua vyuma vizito ambalo husaidia misuli kuinuka, kukua na kuongezeka ukubwa na nguvu.
Zoezi la kwanza
Wataalam wa mambo ya mapenzi wamethibitisha zoezi la misuli ya uume ambalo ni sehemu ya “physiotherapy”ndiyo hurudisha uwezo wa nguvu za kiume kiasili, zoezi hili halina madhara yoyote kiafya na linaweza kufanyika wakati wowote.
Jinsi ya kufanya zoezi hili
Ukiwa umekaa popote fanya zoezi hili asubuhi na jioni ukiwa katika hali ya kutokuwa na mkojo kabisa (yaani kojoa kwanza)
Ukiwa umekaa anza kujibana kama mtu aliyebanwa na mkojo halafu choo kipo mbali ( kama vile unabana haja ndogo isitoke), bana ili mkojo usikutoke kwa kukaza misuli hiyo ya sehemu nyeti, fanya mara 20>25 asubuhi na jioni kila unavyobana hesabu 3 mpaka 5 kisha unaachia, unabana tena hivyohivyo.
Endelea na zoezi hilo kiasi cha wiki, baada ya wiki mbili ongeza ubanaji zaidi kutoka mara 20 mpaka 70 endelea kufanya zoezi hili kwa wiki 6 na matokeo mazuri huanza kuonekana wiki ya 4 mpaka 6
Comments
Post a Comment