Vijue vyakula hatari kwa kupunguza nguvu za kiume
Vijue vyakula hatari kwa kupunguza nguvu za kiume
Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa.
Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo:
Mbegu za Flax (Flax seeds): vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake.
Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi ya soya. Kama bado unafikiria kula vyakula vilivyo na mbegu za flax ili upate omega-3 achana na wazo hilo. Kama unataka kupata omega-3 kula samaki wenye mafuta mafuta (fish oils) utapata omega-3 ya kutosha.
Licorice: Huu ni mzizi ambao hutumika hasa kuondoa tatizo la msongo (stress) kwa watu wanaokumbwa na tatizo hilo. Pia mzizi huo hutumika kama sukari kwenye vinywaji kama chai au kahawa badala ya kutumia sukari ya kawaida.
Hata hivyo mzizi huu una estrogen ambayo hushusha kiwango cha homoni ya kiume ya testosterone kwa wanaume. Kuna utafiti ulifanywa ambapo wanaume 7 wenye afya walipewa gramu 7 za vidonge vya licorice kila mmoja kila siku.
Vidonge hivyo vilikuwa na kiasi cha gramu 0.5 za glycyrrhizic (kiambata kilichomo ndani ya licorice kinachopunguza testosterone kwa mwanaume). Baada ya siku 4 tu kiasi cha homoni ya testosterone kwa kila mwanaume aliyefanyiwa utafiti huo kilipungua kwa kiwango cha nusu ya kiasi cha homoni kwa kila mwanaume kilivyokuwa wakati wa kuanza utafiti.
Bia (Beer): Sipendi kusema habari mbaya kwa wanywaji wa bia. Hata hivyo ni vema kusema ukweli kuhusu athari ya bia kwa wanaume. Bia imetengenezwa kwa humle (hops) ambayo kwa kiwango kikubwa inaleta hali ya homoni za kike kwa wanaume (highly estrogenic).
Humle (Hops) ina kiasi cha 300,000 IU cha estrogen kwa kila gramu 100 za hops. Kabla ya mwaka 1487 bia ilikuwa ikitengenezwa kwa viambata (ingredients) ambazo zililenga kuifanya bia inaponywewa na mwanaume humfanya mwanaume awe na hali ya uanaume kweli kweli (more aggressive, horny, and socially dominant).
Hata hivyo baadaye Kanisa liliingilia uzalishaji wa bia na kutaka bia itengenezwe kwa viambata ambavyo vitamfanya mwanaume awe mpole au mtaratibu na sio mtu wa maguvu na ubabe ( to make men more feminine and sensitive). Hapo ndipo likazaliwa wazo la kutengeneza bia kwa kutumia humle (hops). Siku hizi bia hutengenezwa kwa viambata vitatu, hops, maji na malt.
Soya (Soy): Ina kiwango kikubwa cha Isoflavones ambayo ni kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango (birth control pill). Kwa kuelewa zaidi madhara ya soya kwa wanaume soma hapa.





Comments
Post a Comment