Saikolojia inavyotibu tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni!

Saikolojia inavyotibu tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni! Miongoni mwa matatizo makubwa kabisa yanayowakabili wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kuwa, wanaume saba kati ya kumi wanakasoro hii. Malalamiko yanayotolewa na baadhi yao yanaonesha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba. Hata hivyo, kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la pili na kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya wanawake limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi. Ni ukweli usiopingika kuwa, mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani humwacha njia panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana. Hali hii inatokana na maumbile ya uume wa mwanaume ambao husinyaa mara baada ya kuhitimis...